960 3-Column PSD Grid Template
Jana tulishuhudia timu ya Simba na Coastal union zikikabana koo katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara katika mchezo uloisha kwa timu hizo kugawana point.Mpaka  dakika 90 refa Jacob Adongo anapuliza kipenga kuashiria kumalizika kwa mchezo huo timu hizo zilikua zimefungana  bao 2-2.
Nilibahatika kufanya mahojiano mafupi na kocha wa Simba ili kupata maoni yake kuhusu mechi hiyo.
SAM_0480
MAHOJIANO YANGU NA KOCHA PHIRI
Mwandishi:Kocha unauzungumziaje mchezo kwa ujumla.
PHIRI:Mchezo kwetu ulikua mzuri na kiukweli ulikua upande wetu,Ila mipango yetu iliharibika baada ya Haruna Chanongo kuumia.
Mwandishi:Kocha kwa hiyo wewe hauna ‘plan B’ ya mchezo maana kwa kawaida nimeona makocha na timu nyingi duniani kila mchezaji anakuwa na mbadala wake sahihi jambo ambalo kwako hauna
PHIRI:Hapana ,Uhuru ndio ‘plan B ‘ yenyewe ingawa alishindwa kufanya aliyokua anafanya Chanongo.
Mwandishi:Ko cha inaonekana safu yako ya beki imekosa mtu kama Mussoti huoni kuachwa kwa Mussoti ni tatizo kwa Simba.
PHIRI: Mussoti ni mchezaji mzuri ila wapo wengi wazuri ambao wanaweza kucheza nafasi aliyokua akicheza vizuri sana.
Mwandishi:Kocha unaongeleaje mechi ijayo dhidi ya polisi
Polisi:Polisi ni timu nzuri tutajitahidi kuyarekebisha makosa ya leo ili tushinde mechi  hiyo.
Mwandishi:Kocha ahsante
PHIRI:Karibu
Na Allen kaijage

 
Top