WAKATI huu Manchester United haichezi mashindano ya ulaya, David de Gea na baadhi ya wachezaji wenzake wanafurahia mapumziko mafupi ya katikati ya wiki na kula bata tu.
Kipa huyo wa Hispania aliposti picha yake akiwa katika chakula cha usiku na Marcos Rojo, Rafael, Antonio Valencia, Andreas Pereira, Anderson, Angel di Maria, Ander Herrera na Juan Mata.
Kipa huyo wa zamani wa Atletico Madrid aliposti picha katika akaunti yake ya Twita akisema: ‘Chukula cha usiku na timu’