SIMBA6
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Mrisho Ngassa (17), akimpiga chenga aliyekuwa beki wa  Simba, Mkenya, Donald Mtosi wakati mchezo wao wa Nani Mtani Jembe mwezi Desemba  mwaka jana
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Wakati uongozi wa Simba ukidai kuwa bado una mkataba na beki Mkenya Donald Mosoti, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeitaka klabu hiyo kumlipa fidia beki kwa kuwa mkataba wake umevunjwa.
Katibu Mkuu wa Simba, Stephen Ally alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini jana akisema kuwa Mosoti bado ni mchezaji wao halali kwa vile mkataba kati yao na mchezaji huyo badi haujavunjwa.
Donaldi Mosoti akiwa kazini enzi zake Simba sc
Klabu hiyo kongwe nchini, iliamua kumwacha beki huyo dakika za mwisho za usajili msimu huu ili kumsajili Emmanuel Okwi aliyevunja mkataba wake na Yanga huku mwanasheria wa Mosoti, Felix Majani akidai kuwa uamuzi huo ulifanywa bila kumshirikisha mteja wake.
Mwanasheria huyo anayeishi Ureno amekaririwa na mtandao wa Futaa.com wa Kenya leo asubuhi akieleza kuwa ilibidi kuvunja mkataba wa Mosoti na Simba kwanza kabla ya kulifikisha mbele ya FIFA kwa kuwa Simba walikuwa bado wanadai kwamba Mosoti ni mchezaji wao na walitaka aidha wamuuze au kumtoa kwa mkopo.
Majani amesema kuwa mteja wake anataka Simba imlipe fidia kwa kuvunja mkataba wake ilhali alikuwa bado ana muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu kuitimkia klabu hiyo ya Msimbazi. “Kimsingi Mosoti anataka fidia na ameomba adhabu za kisoka zichukuliwe dhidi ya Simba, kwa kufungiwa kusajili wachezaji kwa misimu miwili ijayo ya usajili na tayari FIFA imeshauandikia barua uongozi wa Simba kuukumbusha juu ya kesi hii,” amesema Majani.

 
Top