Maamuzi mabaya: Rio Ferdinand anaamini Man United wanaweza kujuta kumuuzaDanny Welbeck
BEKI wa zamani wa Manchester United,Rio Ferdinand amekiri kushangazwa na maamuzi ya Louis van Gaal kumuuza Danny Welbeck kwa wapinzani wao wa ligi kuu, klabu ya Arsenal.
Welbeck aliyetokea katika akademi ya Manchester United aliuzwa Emirates siku ya mwisho ya dirisha la usajili majira ya kiangazi kwa dau la paundi milioni 16 baada ya Van Gaal kuona nyota huyo wa kimataifa wa England hatakuwa na namba Old Trafford.
Mkongwe huyo alisema hata kama Welbeck alifanya vizuri, Wayne Rooney na Robin Van Persiea walimfanya asionekane kitu kwa United.
Ferdinand akiongea na gazeti la The Sun la jumapili, alizungumzia kitendo cha Welbeck kujiunga na Arsenal: “Siamini kama United wamemruhusu Welbeck kuondoka, hususani kwenda Arsenal. Kwa upande wangu naona ni kuchanganyikiwa”.
“Ni mchezaji hatari kwa mabeiki na kama Arsenal watamtumia kiusahihi, atakuwa mtu hatari kwao”
“Nadhani hakuonekana sana United kwasababu hata kama alifanya vizuri, Robin van Persoe na Wayne Rooney walikuwa mbele yake. Sitashangaa kuona wanajutia kutombakisha Danny”.
Mechi ijayo, Ferdinand atakutana na Man United kwa mara ya kwanza tangu alipomaliza miaka 12 kuichezea klabu hiyo na kujiunga na QPR.