Klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu
Turiani imeendelea na rekodi nzuri ya mwanzo mzuri wa ligi kwa kushinda mechi
zake zote tatu za mwanzo.
Ikicheza katika uwanja wake wa
nyumbani wa Manungu, Mtibwa Sugar leo imefanikiwa kushika uongozi wa ligi na
kuiengua Azam FC baada ya kuifunga JKT Mgambo kwa 1-0.
Mtibwa ambayo mechi yake ya kwanza
iliiadhibu Yanga 2-0, kabla ya kuwakandamiza ‘Wazee wa kukatiza mapori’ Ndanda
FC 3-1, sasa imefikisha jumla ya pointi 9 katika msimamo wa ligi Vodacom
Premier League.
Goli la Mtibwa Sugar leo lilifungwa
na mchezaji Ally Shomari dakika 10 baada ya mchezo kuanza.