7
Watu wanaweza kusema Simba si timu bora, kuliko ile ya msimu uliopita walipomaliza katika nafasi ya nne. Sivyo, labda wanachotakiwa kufanya sasa ni kupambana wote kama timu, kuhakikisha umoja wao unarudi kikosini. Kama dhamira ya makundi yote klabuni ni moja, basi lazima kila mmoja kupambana kuhakikisha timu hiyo inarejea katika kiwango chake cha kawaida.
bukoss11-546x291
Kama kuna makundi ni vigumu kufanikiwa katika jambo lolote. Hakuna tatizo kubwa kwa timu hiyo kwa sababu wamekuwa wakicheza, wakitengeneza nafasi na kufunga mabao, walifunga mabao mawili dhidi ya Coastal na wakafunga bao katika kila mchezo dhidi ya Polisi Morogoro na Stand United. Kama wachezaji wazoefu watakuwa wakitoa maelekezo mazuri kwa wachezaji vijana na kuwa na mawazo yenye kufanana.
Simba ni lazima wakubali kuwa katika kikosi chao kuna wachezaji wengi wachanga ambao wanahitaji kupewa uzoefu na wachezaji wazoefu. Uwepo wa wachezaji kama Ivo Mapunda, Nassoro Chollo, Joseph Owino, Amri Kiemba, Uhuru Suleimani usiwe na faida moja tu ya kuwatumia ndani ya uwanja badala yake wachezaji hao wazoefu wanaweza kuwasaidia vijana kama William Lucian, Mohammed Hussein, Hussein Shariff, Manyika Peter Manyika, Miraj Adam, Abdi Banda, Jonas Mkude, Abdallah Seseme, Ibrahim Twaha, Said Ndemla, Ramadhani Singano, Joram Mvegeke, Isihaka na wengineo kuwa na maendeleo katika mbinu zao za uchezaji.
IMG_1391-546x291
Majukumu ya wachezaji yapo wazi. Nina hakika wachezaji wa Simba wanaweza kubadilisha hali ya mambo licha ya kwamba jambo hilo litakuwa gumu na halitakuja kwa uharaka. Kama watarejea katika mchezo ujao wakiwa na nguvu tofauti na waliyoanza nayo, wakiwa na kocha makini ni wakati wa wachezaji kufanya jitihada zaidi na kumaliza makundi yaliyopo ili kuisaidia timu hiyo kama wanavyotaraji mashabiki wa timu yao.
s10
Bado hawajaanza vibaya, bila sha Phiri atakuja na mawazo mapya na kila mchezaji anatakiwa kupambana ili kupata nafasi katika kikosi cha kwanza. Pamoja na safu ya ulinzi kuonekana ‘ kulega lega’ , si sawa kuwalaumu walinzi peke yake badala yake wachezaji wanatakiwa kucheza kama timu. Ulinzi ni kazi ya kila mchezaji uwanjani. Kutoka kwa Tambwe hadi kwa Owino, wachezaji wote wanatakiwa kulinda kama timu. Ulinzi si majukumu ya mchezaji mmoja au wawili katika timu, kama Simba watendelea kucheza na kuacha majukumu yote ya ulinzi kwa wachezaji wachache wataendelea kufanya vibaya. Warudishe umoja, mshikamano, upendo, na ushirikiano vinginevyo wataendelea kuanguka.

 
Top