BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limesema michuano ya Chalenji itafanyika mwishoni mwa mwa huu.
Rogers Mulindwa, Ofisa Habari wa Cecafa, ameririwa na mtandao wa MTNFootball.com leo asubuhi akieleza kuwa ingawa bado wanapambana kupata nchi mwenyeji, michuano hiyo itafanyika Desemba mwaka huu.
“Baada ya kujiondoa ghafla na ambako hakukutarajiwa kwa Ethiopia kuwa mwenyeji wa mashindano, kwa sasa tupambana kwa nguvu zote kujaribu kupata nchi mwenyeji na Desemba ndiyo mwezi pekee tunaoweza kuutumia kwa michuano hiyo,” Mulindwa amesema.
Ameeleza kuwa kwa vile michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2015 itafanyika Januari, itakuwa busara kwa Cecafa kuendesha michuano ya Kombe la Chalenji Desemba. “”Kwa kweli si kazi rahisi katika hali ya sasa kupata nchi mwenyeji lakini tunapambana kufanikisha hilo,” amesema Mulindwa.
Michuano hiyo ingeweza kuzipa wakati mzuri timu za taifa za ukanda wa Cecafa ambazo hakuna hata moja iliyofanikiwa kufuzu fainali zijazo za Afcon 2015. Mabingwa mara 13, Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) wanatarajiwa kushiriki pamoja na mabingwa watetezi, Kenya. Nchi nyingine ni Tanzania, Sudan, Sudan Kusini, Zanzibar, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia na Djibouti.
Tayari Taifa Stars na Zanzibar Heroes zimeshavunja kambi baada ya Cecafa kushindwa kuthibitisha uwapo ama kutowapo kwa michuano hiyo mwaka. Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na ule wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) umeshaweka wazi kwamba utazirudisha kambini timu zake za taifa endapo Cecafa ikipata mwenyeji mpya wa michuano hiyo, hata hivyo.