RAIS Evansi Aveva wa klabu ya Simba umeiambia Goal matumaini ya timu yao katika msimu huu yatabaki wa washambuliaji watatu wa kimataifa ambao ni Emmanuel Okwi,Amisi Tambwe na Raphael Kiongera na Mtanzania Elias Maguli. Hawatakuwa na nafasi ya kusajili mchezaji kutoka nje ya Tanzania.
Aveva ameiambia Goal, anaimani na wachezaji hao na ndiyo maana kocha wao Mzambia Patrick Phiri amependekeza usajili watakao fanya kuzingatia eneo la kiungo na ulinzi ambayo yamekuwa na mapungufu makubwa tangu kuanza kwa msimu huu.
“Tuta sajili wachezaji katika dirisha dogo lakini siyo katika nafasi ya ushambuliaji bado kocha pamoja na sisi viongozi tunaimani na wachezaji tuliokuwa nao naamini wataisaidia Simba kufanya vizuri ligi itakapo endelea,”amesema Aveva.
Simba wanashindwa kusajili wachezaji kutoka nje kwa sasa kwa kuhofia kupata garama kubwa ya kuvunja mikataba ya waliopo kwa sasa ambao ndiyo kwanza wamewasajili na bado wanaimani nao watafanya vizuri licha ya baadhi yao kukabiliwa na majeruhi.
Awali zilikuwepo habari kuwa huenda Simba ikawatupia virago wachezaji Amisi Tambwe rai wa Burundi na Raphael Kiongera Mkenya aliye sajiliwa msimu huu akitokea Gor Mahia kutokana na kuonyesha mchango ndani ya timu hizo na nafasi zao kuchukuliwa na Mganda Danny Sserunkuma na Mnigeria aliyewahi kuichezea Simba siku za nyuma Emeh Izuchukwu.