Manchester United's van Persie celebrates with his teammate Falcao after scoring  a goal against West Ham United during their English Premier League soccer match at Old Trafford in Manchester
By Aidan Charlie Seif
Robin van Persie alisajiliwa na Sir Alex Ferguson kumsaidia kuurudisha ubingwa wa England Old Trafford kutoka kwa mahasimu wao Manchester City. Alifanya hivyo kwa kufunga magoli 26 katika mechi 38, mchango mkubwa katika msimu wake wa kwanza. Van Persie mpaka sasa amefunga magoli 41 katika mechi 70 za ligi, idadi nzuri, lakini kiwango chake kimekuwa kikishuka tangu amsimu uliopita.
Msimu uliopita alikuwa anaonekana hayupo fiti na ingawa rekodi yake ya magoli ilikuwa nzuri, magoli 12 katika mechi 21, ila tayari alishaanza kuonyesha kushuka kiwango. Pamoja na hayo pia ikaripotiwa kuwa hakuwa na na mahusiano mazuri na kocha wa wakati huo David Moyes. Ujio wa Louis van Gaal ulitoa matumaini kwamba angerudi kwenye kiwango chake, kwa kuzingatia kwamba wawili hao wana uhusiano mzuri wa kikazi, Van Gaal akitokea kuwa kocha wa timu ya taifa ambayo Van Persie alikuwa nahodha.
Msimu huu amekuwa na kiwango kibovu kupita maelezo. RVP ameanza katika mechi 11 za Premier League msimu huu lakini amefunga magoli 3 tu. Pamoja na Van Gaal kumuonyesha kwamba anamuamini lakini bado ameshindwa kurudisha makali yake. Van Persie amejaribu kufunga mara 26 msimu huu,  hivyo inamaanisha kwamba ametumia vizuri asilimia 11 tu ya nafasi alizopata, uwiano mdogo kwa mashambuliaji wa aina yake. Alicheza ovyo sana dhidi ya Arsenal, akishindwa kuwa na impact yoyote kwenye mechi . Aligusa mpira mara 12 katika dakika 75 alizocheza uwanjani. Unaweza kuona kwenye ramani ya mchezo wake hapo chini.
 
Top