Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope umetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango mkongwe wa timu hiyo Juma Kaseja.
Akizungumza na kipindi cha Sports Leo cha Radio One, Hans Pope amesema hawatomuongezea mkataba Kaseja na wamempa baraka za kutafuta timu nyingine.
Kwa muda mrefu Simba ilikuwa ikisuasua kumpa mkataba Kaseja aliyeidakia Simba kwa takribani miaka 10, na hatimaye leo wamethibitisha rasmi kumuacha Kaseja.
Kwa hanari zaidi kuhusu suala hili endelea kufuatilia mtandao huu.
0 maoni:
Post a Comment