SHEKHE Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali(kama inavyoonekana pichani chini) na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha. Sheikh Makamba ambaye amelazwa
SHEKHE
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa
maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa
nyumbani kwake jijini Arusha.
Shekhe
Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa
Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni
huku akiendelea na matibabu.
Akizungumza
kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana
nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka
kuswali Swala ya Tarawei.
Shekhe
Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya
swala hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao
walikuwa wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala.
Alisema
hata hivyo, kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba
wakati akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu
akiwa amesimama jirani na mlango.
Alieleza
kuwa wakati akitaka kumwangalia zaidi alishtukia mtu huyo akiinua mkono na
kumwagia maji yaliyompatia maumivu makali usoni na kifuani.
‘’Wakati
natoka msalani nikipitia uwani kwangu niliona kama mtu ameinama pembeni yangu
wakati najaribu kumsogelea ili nijue ni nani nilihamaki mtu huyo akinimwagia
maji yaliyonisababisha maumivu makali sana yenye asili ya moto na ngozi kuanza
kubabuka,’’ alisema shekhe huyo.
Aliongeza
kuwa baada ya tukio hilo alianza kupiga kelele kuomba msaada ambapo majirani
walijitokeza na kumpa msaada wa kumpeleka hospitali, kwa vile wakati huo macho
yake yalikuwa hayaoni na wakati wote alikuwa akilia.
Pamoja
na kujeruhiwa vibaya sehemu za usoni, kifuani na mgongoni, pia ana majeraha
kwenye mikono na machoni na hali yake bado ni mbaya japo madaktari wanaendelea
kumpatia matibabu.
Kaimu
Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud akizungumzia tukio hilo
alieleza kushitushwa nalo akisema limefanana na lile la Katibu wa Bakwata Mkoa
wa Arusha, Abdulaziz Jonjo ambaye mwaka jana alilipuliwa kwa bomu nyumbani
kwake akiwa amelala.
Alisema
kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia huku wahusika wakishindwa kutiwa mbaroni
na kudai kuwa matukio hayo yanahusiana na masuala ya kigaidi.
Aliongeza
kuwa pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, lakini wamekuwa hawapati
matunda ya kukamatwa kwa watuhumiwa ingawa alisema wanajulikana.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi
wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zitatolewa pindi washukiwa
watakapotiwa mbaroni kwani uchunguzi bado unaendelea na kwamba hakuna mtu
anayeshikiliwa hadi sasa.
0 maoni:
Post a Comment