BAADA YA SUAREZ: SASA WAYNE ROONEY NAE AONDOLEWA KUFANYA MAZOEZI NA KIKOSI CHA KWANZA CHA UNITED - APELEKWA KIKOSI CHA PILI

Siku moja baada ya Liverpool kumuondoa Luis Suarez kama mazoezi ya kikosi cha kwanza na kumlazimisha kufanya mazoezi pekee yake, leo hii Wayne Rooney nae amefanyiwa kitendo hicho hicho na kocha wake wa Manchester United David Moyes kwa kumpeleka mshambuliaji huyo anayetaka kuondoka kufanya mazoezi na kikosi cha pili cha timu ya mabingwa wa England. 

Rooney alikuwa ndio mchezaji pekee wa kikosi cha kwanza kilichokuwa kikifanya mazoezi na wachezaji wa ziada katika uwanja wa mazoezi Carrington, in a session chini ya usimamizi wa makocha Warren Joyce na Nicky Butt.

Mchezaji huyo anayetakiwa kwa udi na uvumba na Chelsea leo alienda mazoezini asubuhi akitegemea kufanya mazoezi na wachezaji wenzie wa kikosi cha kwanza lakini akaondolewa na Moyes na kupelekwa wanapofanya mazoezi wachezaji wa kikosi cha pili.

0 maoni:

Post a Comment

 
Top