BREAKING NEWS: FABREGAS AIKATAA RASMI MAN UNITED - ASEMA ANAHESHIMU KUMHITAJI KWAO LAKINI ANA FURAHA BARCELONA NA ANGEPENDA KUBAKI.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Kuala Lumpur mahala ambapo Barcelona wapo kwa ajili ya maadalizi ya msimu mpya.
Fabregas alisema: 'Ndoto yangu siku zote imekuwa kuichezea Barcelona na hakuna kilichobadilika. Nina furaha sana kuwa hapa na sijawahi kufikiria kuhusu kuondoka.
"Sijawahi kuwa na shaka juu hilo. Haijanigharimu chochote kurudi Barcelona na sasa nataka kuwa mshindi nikiwa hapa.
'Ni heshima kubwa kwa Manchester United kuleta ofa mbili kwa ajili yangu, lakini hakujawahi kuwa na mazungumzo. Sijawahi kuongea na klabu yoyote tangu nimejiunga na Barcelona miaka miwili iliyopita.
'Siku zote nimekuwa nikitambua ninavyothaminiwa na klabu. Kila mut ameniambia namna anavyonitegemea, sijwahi kupata ishara yoyote tofauti ya kuhisi sihitajiki.
'Sikutaka kusema lolote huko mwanzo kwa sababu kwangu mimi kila kitu kilikuwa wazi kwamba nilikuwa nataka kuendelea kubaki hapa. Niliiambia klabu nitaongea itakapofika zamu yangu.
'Kuna baadhi ya vitu vilitengenezwa, lakini havikuwa vya kweli - hasa la kusema kwamba nimeomba kuongezewa mkataba,' alisisitiza Cesc Fabregas
0 maoni:
Post a Comment