GERRARD: "SITEGEMEI SUAREZ KUONDOKA ILA KAMA AKIONDOKA BASI ITAKUWA NJE YA UINGEREZA "Suarez U-turn: I'm staying at Liverpool

Nahodha wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard amezungumza na kusema mchezaji mwenzie wa klabu hiyo Luis Suarez hatoruhusiwa kujiunga na klabu ya kiingereza. 

Arsenal tayari inaaminika walishatuma ofa mbili ambazo zimekataliwa kwa ajili ya kupata huduma za mruguay huyo na Suarez amepewa adhabu ya kufanya mazoezi pekee yake na kocha wa Liverpool Brendan Rodgers baada ya kuituhumu klabu hiyo kuvunja ahadi ya kumuuza endapo watashindwa kufuzu kucheza Champions League. 

Akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Scotland, Gerrard alisema angependa kumuona mshambuliji huyo mwenye 26 anaendelea kuwepo Liverpool. 

"Nadhani ni muhimu kwa Suarez kubaki. Ni mmoja wa wachezaji bora duniani na naelewa vizuri kwamba klabu nyingi zinamtaka," Gerrard alisema.
"Ikiwa nitatumia nguvu ya ushawishi wangu kumfanya abaki basi nitafanya hivyo, kwa sababu napenda kucheza nae timu moja na sitaki kumuona akiondoka. Kwa Liverpool ili ifanikiwe kwenda mbele zaidi inabidi tujitahidi kubaki na wachezaji wetu bora."
Alipoulizwa ana matumaini gani juu ya kubaki kwa Suarez, Gerrard alijibu: "Kwa sasa hivi, sina ninachojua. Huo ni ukweli kabisa, sijui nini kitatokea wiki kadhaa zijazo zilizobakia za usajili, lakini nina uhakika sana kwamba hata kama ikitokea imeuzwa basi haitokuwa kwa klabu yoyote nchini England."

0 maoni:

Post a Comment

 
Top