WAKAZI WA KIGOMA WALIPOKEA KWA KISHINDO TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia kwenye jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta 2013,usiku huu kwenu uwanja wa Lake Tanganyika.
Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu wakiburudika na Wasanii wa Serengeti Fiesta 2013
Burudani ya kutosha kabisa
Hapatoshi ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu.
Mwanamuziki mahiri wa muziki wa Dansi,Christian Bella akikamua jukwaani usiku huu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,mkaoni Kigoma ambapo watu wamefurika ile mbaya.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akiimba jukwaani mbele ya maelfu ya wakazi wa Kigoma ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
Sehemu ya umati wa watu waliofurika ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu
Msaniii anekuja kwa kasi kwenye miondoko ya Hip Hop,Stamina akikamua jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta
Ni Shangwe tu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma usiku huu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea
Yaani hapatoshi kabisa,wakazi wa Kigoma wamecharuka na burudani murua kabisa ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael kutoka THT,akionesha umahiri wake wa kutumbuiza jukwaani usiku kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Washabiki wa tamasha la Fiesta wakifuatilia kwa makini yanayojiri usiku huu ndani y uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Wadau nao wamejitokeza kwa wingi
Peter Msechu na densa wake wakikamua vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Pichani ni msanii wa bongofleva akulikanae kwa jina la Shilole na madansa wake wakiwachengua vilivyo wakazi wa Kigoma,waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
0 maoni:
Post a Comment