Ishu hiyo ilianza tangu mwanadada huyo maarufu kama Kiuno Bila Mfupa alipohojiwa kupitia CloudsTV ambapo alieleza jinsi alivyofiti kiafya.

“Unajua tangu aliposema anamshukuru Mungu kumuepusha na shetani wa madawa ya kulevya, wanaume kibao wamekuwa wakimfuatilia wakitangaza dau la kumuoa.

“Lakini pia kilichochochea zaidi wanaume kutaka kumuoa ni pale aliposema amepima Ukimwi na yupo fiti kabisa kiafya.

“Kama hamuamini fuatilieni akaunti yake kwenye Instagram (mtandao) muone. Kila akiweka picha mpya kwa ajili ya mashabiki wake kinachofuata ni maombi ya wanaume wanaomsifia kuwa ni mzuri.

“Yaani wanaume wanamwaga ahadi kibao kama kumjengea mjengo wa kifahari, kumnunulia magari, kila mmoja akimhakikishia maisha bora katika ndoa,” kilisema chanzo chetu.

Gazeti lilipoperuzi kwenye akaunti hiyo ya Ray C na kukutana na maombi hayo ya wanamme.

Katika mahojiano yake na CloudsTV, Ray C alisema kwa sasa hawazi kitu kingine tofauti na kurudi kwanza kwenye muziki kwa kishindo.

0 maoni:

Post a Comment

 
Top