SHAHIDI WA TANO AELEZA ALIVYOLAZIMISHWA KUZINI NA MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG
SHAHIDI wa tano katika kesi ya kutorosha wanafunzi inayomkabili Mchungaji wa Kanisa la TAG, raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC), Jean Felix Bamana ameieleza mahakama namna alivyolazimishwa kufanya mapenzi na mchungaji huyo.
Shahidi huyo, Angela Swai (19), akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu, Naomi Mwerinde wa Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, alisema Mchungaji huyo alimlazimisha kufanya kitendo hicho jaribio ambalo lilishindikana kutokana na mshitakiwa huyo kukataa kutumia kondomu.
Akiongozwa na mwendesha mashtaka, wakili wa serikali, Esther Majaliwa, katika ushahidi wake, Shahidi huyo alieleza Mahakama hiyo alivyokutana na mshtakiwa kwa mara ya kwanza na mara ya pili ambapo alisema alikutana naye kupitia marehemu mama yake mzazi huku mara ya pili akikutana naye kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Shahidi huyo alieleza mahakamani hapo kuwa alikutana na mshtakiwa kwa mara ya kwanza kupitia mama yake na alimtambulisha yeye na mdogo wake aliyemtaja kwa jina la Arthur kuwa mchungaji huyo ni baba yao mwingine na waliendelea kufahamiana kwani alikuwa ni rafiki mkubwa wa mama na mshirika wake katika Biashara ya Madini.
Alisema kwa kipindi kirefu hakuwahi kumuona hadi alipokutana naye kwa mara ya pili mwaka jana kupitia mtandao wa Facebook ambapo alimwomba urafiki kwa nia njema kwani alikuwa ni rafiki mkubwa wa marehemu mama yake, na kuongeza kuwa mawasiliano yalikuwa ni ya kawaida tu.
Shahidi huyo alisema baada ya hapo mshtakiwa alianza kumsisitiza kuhamia Dar es Salaam kwa ahadi ya kumsaidia kuendelea na masomo baada ya kumueleza amefukuzwa shule jambo ambalo yeye binafsi alilikataa.
Alisema baada ya kukataa kukubaliana na wazo la kwenda Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alimwambia atafika Moshi ambapo alifikia katika Hoteli ya Moshi View, Februari 14, mwaka huu na kufanya naye mawasiliano kupitia simu ya mdogo wake aliyetajwa mahakamani hapo kwa jina la Arthur Swai, akimtaka kumfuata hotelini hapo.

0 maoni:
Post a Comment