Ander Herrera ameonyesha wazi kwamba yupo tayari kujiunga na Manchester United mnamo mwezi January. 
Kiungo huyo wa Athletic Bilbao alikuwa akitakiwa na United na ikatumwa ofa ya £26m kwa ajili ya kumnunua na ikapigwa chini na Bilbao - huku wakisisitiza mchezaji atauzwa mara tu United watakapolipa kiasi cha £30.5m ili kuvunjamkataba wao na mchezaji huyo. 
 
Herrera, 24, alisema: 'Ilikuja ofa kutoka kwa United na naweza kuona hilo ni jambo zuri kwa maana wamevutiwa na kiwango changu. 
'Pamoja na kuripotiwa nilifanya vipimo vya afya au kukubaliana na United, lakini chochote kilichotokea baina yangu na klabu hiyo. Ukiniuliza kuhusu usajili huko mbeleni, lolote linaweza kutokea.'
 
Herrera pia amewakana kabisa wanasheria watatu ambao walifika kwenye ofisi za La Liga kwenda kufanya mazungumo juu ya kipengele cha kuvunja mkataba wamchezaji huyo na Bilbao. 

'Sina uhasiano wowote na wale watu watatu ambao walienda kwenye ofisi za ligi - na naweza kusema hawakuwa na lolote kwa pamoja na wawilikilishi wangu.'

0 maoni:

Post a Comment

 
Top