Usije kushangaa pale ambapo utamuona Rapper Stamina mtaani kwako akifanya shughuli za kijamii, kwasababu hivi sasa ameamua kuanzisha taasisi yake binafsi (NGO) aliyoipa jina la Kabwela Foundation.
"Ni Foundation ambayo nimeianzisha yaani ni kampuni kabisa ambayo tayari nimeshaisajili, na itakuwa inajihusisha zaidi na maswala ya kijamii, hasahasa kuwatembelea walemavu, maana kumekuwa na taaisisi nyingi ambazo zimekuwa zikiwaangalia sana watoto yatima, sasa mimi nitakuwa nikiwaangalia zaidi walemavu, sio yatima, kuna walemavu wana wazazi wao lakini hawajiwezi" amesema Stamina
hata hivi aliongeza kwa kusema mpaka sasa tayari ameshapata atakaokuwa akishirikiana nao ambao ni wasanii wenzake, Young killer, G Warawara, Joe makini pamoja na Godzilla, ambapo atakuwa akitembelea kituo kimoja katika mkoa mmoja kila mwisho wa mwezi, na baada ya miezi 12 atakuwa ametembelea mikoa 12.
All the Best Stamina, watu kama wewe ndio wanaohitajikakatika jamii..Big up.
0 maoni:
Post a Comment