Leo September 2 ya mwisho ya dirisha la usajili barani ulaya - vilabu kadhaa vimekuwa busy katika siku hii kuhakikisha wanaimarisha timu zao. Mtandao huu utakuwa unakuletea taarifa zote zinazohusiana na usajili barani ulaya. Ungana nasi.................
TAARIFA ZOTE ZINAZOHUSIANA NA USAJILI BARANI ULAYA
- Manchester United na Everton wameendelea kubishana juu ya ada ya uhamisho wa Leighton Baines - taarifa zilitoka hivi sasa zinasema kwamba Toffes wameikataa ofa ya £15m na wamewaambia United ni kiasi cha£20million ndicho kitawafanya wafanye baishara ya mchezaji huyo.
- Yakiwa yamebaki masaa 6 kabla ya dirisha la usajili kufungwa vyombo vya habari vikubwa vya Spain, Marca na AS vimeripoti kwamba Man United wamekubali kulipa kiasi cha £30.5 kw ajili ya Ander Herrera na kiungo huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka 5 leo hii.
- Wakati kukiwa hakuna taarifa zaidi kuhusu usajili wa Ozil, imefahamika Arsenal wanajiandaa kuongea na PSG kuhusu upatikanaji wa kiungo ambaye amepoteza nafasi katika hiyo Javier Pastore
- Leighton Baines ameruhusiwa kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya England, na kocha Roy Hodgson amesema atamruhusu kuondoka kwa mara moja ikiwa Everton na United watafikia makubaliano kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo.
- Chama cha soka cha Ubelgiji kimethibitisha kwamba Marouane Fellainihatojiunga na timu hiyo ya taifa leo hii na atajiunga na timu hiyo mapema kesho - inaaminika kwamba mchezaji huyo atakuwa bize kukamilisha usajili wake kwenda Manchester United.
- Emmanuel Mayuka amejiunga na Sochaux kwa mkopo baada ya kufeli upata nafasi St Mary's yalipo makao ya Southampton..
- YAMEBAKI MASAA 7 DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA
- Peter Odimwingie anakaribia kujiunga na Cardiff kwa uhamisho wa £2.5m
- Mshambuliaji wa Uturuki Burak Yilmaz anakaribia kujiunga na Lazio €15 million kutoka Galatasaray kwa mkataba wa miaka mitano, hii ni kwa mujibu wa Sky Italia.
- Ikiwa Juan Mata atajiunga na PSG, basi inaaminika Javier Pastoreataruhusiwa kuondoka katika kikosi cha mabingwa wa Ufaransa - alizomewa na mashabiki wa timu yake jumamosi iliyopita.
- Mesut Ozil anategemewa kupewa jezi namba 11 pindi atakapojiunga rasmi na Arsenal.
- Juan Mata anahusishwa kujiunga kwa mkopo na Liverpool au kuuzwa kwenda PSG jioni hii.
- Ander Herrera anakaribia kujiunga na Man United, katika dili ambalo linatarajiwa kukamilika jioni hii kwa mujibu wa mtandao wa Dailymail: Ander Herrera anaaminika amekubali kupunguza mahitaji ya mshahara wake ili kufanikisha dili hilo, ili kuipa nafasi United kuweza kuvunja rekodi ya usajili wao kwa kulipa kiasi cha £30.5million. Mkataba wake na United unategemewa kuwa kiasi cha £3.3millionkwa mwaka - £64,000 kwa wiki - na atasaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo.
- Mshambuliaji Demba BA anatarajia kujiunga na Arsenal baadae leo hii baada ya Gunners kutuma ofa ya £1.5million lakini Chelsea bado wanang'ang'ania kiasi cha £3m.
. Arsenal imekubaliana na Real Madrid uhamisho wa kiungo raia wa Ujerumani Mesut Ozil wenye thamani ya £42.4m.kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 tayari amekubaliana mahitaji binafsi, kwasasa Ozil yupo kwenye kambi ya Timu ya Taifa nchini Ujerumani na anataraji kufanyiwa vipimo vya afya nchini Ujerumani.
Source: bbc
- Fabio Borini anafanyiwa vipimo vya afya na Sunderland. Atajiunga na Sunderland kutoka Liverpool kwa uhamisho wa mkopo. Getafe wamekamilisha usajili wa mkopo wa Lisandro Lopez kutoka Benfica kwa msimu wa 2013-14 season
- Wakati huo huo taarifa kutoka Ufaransa zinasema PSG imeipiku Arsenal na United katika mbio za kumsajili Mesut Ozil kutoka Real Madrid.
Gareth Bale amefuzu vipimo vya afya kujiunga na Real Madrid
- Victor Moses amejiunga na Liverpool akitokea Chelsea kwa mkopo wa mwaka mmoja.
- Ripoti kutoka Spain zinasema kwamba Gareth Bale amefaulu vipimo vya afya na sasa yupo njiani kwenda Santiago Bernabeu kwa ajili ya kutambulishwa. Picha za zoezi zima la utambulishwaji utazipata hapa
- Ricardo Kaka amezungumza kuhusu uhamisho wake wa kurudi AC Milan na amepewa jezi yake ya zamani namba 22.
- Sunderland wanakaribia kukamilisha usajili wa Fabio Borini kutoka Liverpool, wakati Paolo Di Canio pia anafukuzia saini ya mlinzi Andrea Dossena
- Chelsea imekamilisha uhamisho wa winga wa FC Porto Christian Atsu. Atsu amesaini mkataba wa miaka mitano na hapo hapo ametolewa kwa mkopo kunako timu ya Vitesse Arnhem ya nchini Uholanzi hadi mwishoni mwa msimu huu.
- Emiliano Viviano amefaulu vipimo vya afya vya kujiunga na Arsenal kwa mkopo kutoka Palermo.
- Mtandao wa wa GOAL.COM unaripoti kwamba Manchester United na Everton zimekubaliana ada ya uhamisho wa £24m kwa jili ya Maroune Fellaini - dili kutangazwa rasmi muda mchache ujao
- Wawikilishi wa Maroune Fellaini wanasubiri ruhusa rasmi kutoka Everton ili waanze rasmi mazungumzo ya masalhi binafsi ya mchezaji na United.
- Tetesi! Mitandao wa ESPN na SKYSPORTS Inaripoti kwamba baada ya dili la Ozil kwenda Arsenal kukwama - Manchester United nao wameanza mawasiliano na wawakilishi wa Ozil - huku Gunners bado wakiwa hawajakata tamaa kuhusu mchezaji.
- Ripoti zinasema baada ya Mesut Ozil kuikataa Arsenal - klabu hiyo imemgeukia mchezaji wa Saint-Etienne Joshua Guilavogui kwa ada ya uhamisho wa €10 million .
- Everton wapo katika harakati za kuwasajili wachezaji wawili wa Manchester City Joleon Lescott na Gareth Barry, wachezaji wote wawili inaonekana hawana nafasi ndani ya Etihad. City inasemekana wanahitaji kiasi cha £7 million ili Everton iwapate wachezaji wote wawili.
- Niklas Bendtner anaweza kuondoka Arsenal leo hii baada ya miaka miwili ya kuhangaika kuondoka moja kwa moja, mpaka mwisho wa siku hii anaweza akawa amejiunga na Crystal Palace .
Manchester United bado wapo kwenye mazungumzo na Athetic Bilbao kuhusu usajili wa Ander Herrera - na sasa wameipa ofa ya kucheza mechi ya kirafiki na Bilbao katika uwanja wao mpya na mapato yote yataenda kwa klabu hiyo ya Spain.
Liverpool wameshamthibitisha Mamadou Sakho |
Arsenal wanategemewa kutangaza usajili wa kwanza leo hi baada ya kukimilisha vipimo vya afya vya golikipa kutoka Palermo Emiliano Viviano, ambaye kwa sasa anafanya vipimo vya afya jijini London. Kipa huyu alijiunga na Arsenal msimu uliopita wakati kama huu lakini dili likashindikana kumalizika ndani ya muda.
Liverpool wanategemewa kutangaza rasmi usajili wa Mamadou Sakho na Victor Moses baada ya kukamilika kwa vipimo vya afya muda mfupi ujao.
Mesut Ozil amekataa kujiunga na Arsenal na kuamua kubaki Real Madrid kwa mujibu wa gazeti la MARCA lenye uhusiano wa karibu wa klabu ya Real Madrid.
Wakati huo huo Maroune Fellaini inasemekana ameomba uhamisho wa kwenda Manchester United.
Everton wamekubaliana ada ya uhamisho wa mchezaji wa Wigan McCarthy kwa ada ya £12m
Martin Demechelis ameshatambulishwa na City - ametokea Atletico Madrid |
Liverpool wamethibitisha usajili wa Tiago Ilori kutoka Sporting Lisbon kwa £7m |
0 maoni:
Post a Comment