Sakata la usajili wa Gareth Bale limefikia tamati usiku wa jana wakati alipohamiaReal Madrid kwa ada ya uhamisho wa dunia £86million. 
Baada ya mazungumzo ambayo yalidumu kwa wakati wote wa dirisha la usajili, kijana huyu kutoka Wales amejiunga na Madrid kwa mkataba wa miaka sita wenye thamani ya £256,000 kwa wiki na atafanyiwa vipimo vya afya leo Jumatatu asubuhi kabla ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari mchana huu.

Katika kuhakikisha hawamkeri staa wao Cristiano Ronaldo - waliyemsajili kwa £80mmwaka 2009 - Real Madrid wamekaririwa wakisema uhamisho wa Bale umegharimu kiasi cha £78m kwa maana Ronaldo anaendelea kuwa mchezaji ghali zaidi duniani. 

Tottenham manager Andre Villas-Boas alithibitisha kwamba makubaliano ya usajili wa Bale yameshafikiwa dakika kadhaa baada ya kufungwa na Arsenal 1-0 katika mchezo wa Barclays Premier League. 
Bale, ambaye aliwasili jijini Madrid usiku wa jana, alisema: 'Ningependa kushukuru kila mtu ndani ya klabu, mwenyekiti, bodi, wafanyakazi, makocha na wachezaji - lakini shukrani kubwa zaidi ziende kwa mashabiki ambao natumaini wataelewa hii ni nafasi adimu kwenye maisha yangu ya soka.
'Sina uhakika kama kuna muda mzuri wa kuihama klabu ambayo nilihisi ni nyumbani wakati nacheza soka. Nafahamu wachezaji wengi huwa wanazungumzia matamanio yao ya kujiunga na vilabu walivyokuwa wakivipenda tangu utotoni lakini kwangu mie naweza kusema kujiunga na Madrid ni kukamilisha ndoto yangu.
'Nisingekuwa hapa nilipo leo kama sio kwa Southampton na baadae Spurs kusimama nami na kunisapoti kwa wakati mgumu. Tottenham siku zote itakuwa kwenye moyo wangu na nina uhakika huu utakuwa msimu wenye mafanikio makubwa kwao. Kwa sasa naangalia mbele kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu ya soka ndani ya klabu ya Real Madrid.' 

0 maoni:

Post a Comment

 
Top