MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya 'Number One', Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' baada ya kutua jijini Dar es Salaam leo akitokea nchini China, alitembelea katika Viwanja vya Leaders ambapo maandalizi ya shoo ya Fiesta 2013 yanafanyika.
Akiwa viwanjani hapo, Diamond aliwataka mashabiki wake wote kuhudhuria shoo hiyo itakayofanyika siku ya Jumamosi Oktoba 26 mwaka huu. Kupitia akaunti yake ya Instagram na tovuti yake, msanii huyo aliandika yafuatayo:
" Kwa heshima ya mashabiki wangu, nchi na taifa langu, ilinibidi nirudi maalumu kabisa kwa ajili ya shoo hii ya Fiesta Jumamosi pale Leaders Club ili kuwakaribisha wageni zetu kutoka nje. Lakini pia kuwadhihirishia wageni hao kuwa Tanzania si legelege imebarikiwa wasanii na wenye uwezo...! Tukutane pale Leaders on Saturday Mdau wangu..."aliandika msanii huyo.
(Picha na Diamond Platnumz)
0 maoni:
Post a Comment