Cristiano Ronaldo amemuondoa Ruud van Nistelrooy katika tatu bora ya ufungaji bora wa muda wote wa ligi ya mabingwa wa ulaya baada ya jana kufunga mabao mawili katika mchezo wa makundi dhidi ya Juventus.
Mshambuliaji huyo wa Los Blancos amekuwa kwenye fomu nzuri msimu katika michuano hii akifunga mabao 7 katika mechi 3 alizocheza. Kwa maana hiyo Cristiano amefikisha jumla ya mabao 57 katika mechi 95 alizocheza katika ligi ya mabingwa wa ulaya.
Cristiano Ronado ambaye sasa ndio mchezaji anayeongoza kwa kufunga mabao mengi katika michuano ya Champions League msimu huu, yupo nyuma kwa mabao 6 kumfikia Lionel Messi anayeshika nafasi ya pili na mabao 14 kumfikia Raul Gonzalez Blanco mwenye mabao 71.

TOP SCORERS UEFA CHAMPION LEAGUE
|
0 maoni:
Post a Comment