Wakati mashabiki wa Manchester United wakionyhesha kukata tamaa juu ya uwezo wa meneja wao mpya David Moyes baada ya michezo saba ya ligi kuu ya England,nyota wa klabu hiyo Wayne Rooney bado ana imani kocha huyo atafanya vizuri kama akipewa muda wa kutosha.
Rooney amesema hakufurahishwa na majukumu aliyopewa na Ferguson msimu uliopita,amekili sasa kuwa na furaha pale Old Trafford sababu kubwa ni Moyes kumchezesha kwenye nafasi anayoipenda ya ushambuliaji tofauti na msimu uliopita ambapo alichezeshwa kwenye nafasi ya kiungo.
‘Kila mtu klabuni alikuwa anajua nafasi niliyokuwa naipenda kucheza,sababu ya mimi kukata tamaa ilikuwa ni kulazimishwa kucheza kwenye nafasi ya kiungo,binafsi sikufurahishwa ila ilinilazimu kucheza kwa ajili ya manufaa ya timu,na ilinibidi wakati furani kuwa mbinafsi ili kunusuru maisha yangu'.
Baada ya mwanzo mzuri sasa nina furaha na nadhani sasa naweza kukaa meza moja na uongozi wa man utd kwa ajili ya kujadili mambo yangu ya baadae.

0 maoni:
Post a Comment