Baada ya kuichapa timu ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika mjini Bukoba mwishoni mwa wiki, jana kikosi cha Young Africans kilirejea jijini Dar es salaam na leo asubuhi kikitua kisiwani Pemba ambapo kitakua kambini kwa muda wa wiki moja.
Young Africans inaweka kambi kisiwani Pemba ikiwa ni mara ya pili mfululizo katika mchezo wake dhidi ya watani wa jadi Simba SC, ambapo kambi ya awali iliwafanya vijana wa jangwani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza 'Diego'.
Msafara wa watu 38 wakiwemo wachezaji wote 29 waliosajiliwa kwa ajili yakuichezea Yanga msimu huu na viongozi 9, watakua kisiwani pemba katika maandalizi ya mchezo huo ambao ni muhimu kwa Yanga ili kujiweka katika mazuri ya kuongoza Ligi Kuu na baadae kuteteta tena Ubingwa wake.
Mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba leo asubuhi kwa ndege tatu za kukodi kikosi kimefanya mazoezi yake ya kwanza katika uwanja wa Gombani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mcezo dhidi ya Simba SC oktoba 20, 2013.
Ikiwa ni takribani siku sita kabla ya kupamba na Simba SC siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kikosi cha mholanzi kimeamua kuweka tena kambi katika visiwa hivyo tulivu kwa lengo la kusaka ushindi.
Kocha Mkuu Brandts amesema anatambua kikosi chake kinakabiliwa na mchezo mgumu, haswa ikizingatiwa wanapokutana watani wa jadi mechi huwa inakua ngumu sana lakini kwa sasa anakindaa kikosi chake ili kiweze kuendeleza wimbi la ushindi.
"Pemba ni sehemu nzuri, tulikuwepo huku mwishoni mwa msimu uliopita kwa ajili ya maandalizi dhdi ya Simba na tuliibuka na ushindi wa mabao 2-0, uwanja wa mazoezi mzuri na hali ya hewa ni nzri vitatutaongeza chachu ya ushindi kufuatia kuwa sehemu tulivu" alisema Brandts
Wachezaji waliondoka kwenda Pemba ni:
Walinda Mlango: Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul.
Walinzi wa Pembeni: Mbuyu Twite, Juma Abdul, Issa Ngao, David Luhende na Oscar Joshua.
Walinzi wa Kati: Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani 'Cotton', Rajab Zahir na Ibrahim Job.
Viungo wa Ulinzi: Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo na Salum Telela na Bakari Masoud.
Viungo Washambuliaji: Haruna Niyonzima, Nizar Khalfani na Hamis Thabit.
Washambuliaji wa Pembeni: Mrisho Ngassa, Saimon Msuva na Abdallah Mguhi 'Messi'
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerson Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Reliants Lusajo na Shaban Kondo
0 maoni:
Post a Comment