KAMA unaweza kufauatilaia historia ya tasnia ya filamu si rahisi sana kumsahau mwigizaji mwasisi katika fani hiyo ya uigizaji Said Wangamba, al maarufu ‘Mzee Small.’Mzee Small anayehitaji msaada wa matibabu lakini kutokana na mfumo uliopo kwa wasanii Swahiliwood, Mzee Small yupo nyumbani tu toka mwezi wa tano mwaka jana bila kutumia dawa yoyote sababu kubwa hana fedha ya kujitibia.
Akiongea na FC mtoto wa kiume wa Msanii huyo ambaye anajulikana kwa jina Mahmud Said Wangamba anasema kuwa pamoja na baba yake kufanya kazi na makampuni makubwa lakini hadi sasa ameshindwa kusaidiwa na kampuni alizowahi kufanya nazo kazi sambamba na Serikali menejimenti ya Umma kwa sasa anasema kuwa anawaona waandishi wa habari tu wakifika kwao.
“Sisi kama familia tunajisikia vibaya sana tunaposhindwa kumsaidia baba kwa sababu yeye ni kila kitu, mimi nasoma sina kipato, mzee toka mwaka jana mwezi wa tano mwaka jana alipomaliza dawa zake hajatumia dawa hadi leo kwa sababu hatuna fedha,”
“Lakini jambo linalotuuma hakuna hata kampuni ambayo imeonyesha kumsaidia kama Bakhresa alikuwa kuwa akifanya nao kazi hakuna msaada lakini pia Serikali kupitia menejimenti utumishi wa umma walikuwa wanafanya nao kazi wamemtosa yupo tu, pengine wanasubiri afe ndio waje kumzika,” anasema Mahmud.
Jambo linaloiuma kama familia ni pale ambapo mwenyekiti wa chama cha waigizaji ambaye anaitwa Chirwa aliposema kuwa chama hicho akiwezi kumsaidia Mzee Small kwa sababu ya kuwa msanii huyo si mwanachama wa chama hicho kitu kinachosikitisha kwa kuzingatia umuhimu msanii kwani inawezekana wazi kuwa kuna hata wasanii wengine waliingia katika fani kwa kumuona yeye.
FC iliongea na mwenyekiti wa chama cha waigizaji Taifa Michael Sangu ‘Mike’ kujua chama hicho kinatendaji shughuli zake katika kujenga umoja na mshikamano katika raha na shida, mwenyekiti huyo alikitishwa na jambo hilo kwa kusema ni kweli kuna utaratibu kama huo lakinikwa msanii kama huyo busara inatakiwa kutumika ili kumsaidia.
“Ni kweli vyama vilifikia kuwa karibu na wanachama kwa sababu wasanii ambao ni chipukizi ndio wamekuwa mbele katika shughuli za vyama lakini wasanii ambao ni nyota wakiwa nyuma kushiriki katika vyama hivi, hivyo kila msanii akawa anahimizwa kujiunga ili kupata msaada, lakini kwa mtu kama Mzee Small busara inatakiwa kutumika na si kumwingiza katika kundi hilo,”anasema Mike.
Mike anasema kuwa vyama vinapaswa kuwa na utaratibu wa kuwa na uanachama wa wa aina mbalimbali ikiwa uanachama wa kutunikiwa kutokana na mchango wa mhusika kama alivyo Mzee Small, uanachama wa heshima na kadharika jambo ambalo Chirwa kashindwa kulifanya Mwenyekiti Mike katika kulinda demokrasia anashindwa kuingilia vyama husika.
Mzee Small ambaye kwa sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ikiwa sambamba na kupoteza kumbukumbu anahitaji zaidi ya milioni moja na nusu kwa ajili ya matibabu kutokana na ushauri wa Daktari kwani inasemekana kichwani kuna tatizo ambalo linamsababishia kupoteza kumbukumbu anahitaji dawa kwa ajili ya tatizo hilo na muda wa kupomzika.
Kwa anayeguswa na tatizo hilo anaweza kuitumia familia yake mchango wa matibabu kwa namba TIGO – PESA 0714 344 039 Baadaye tutakutambulisha namba nyingine ikiwa na utaratibu mwingine kwa ajili ya kumsaidia mzee Small kupata matibabu sisi kama Filamuncentral, Mama Abdul na wadau wengine tunaandaa utaratibu utakao saidia Shujaa huyo kupata matibabu haraka. Chanzo: FilamuCentral
0 maoni:
Post a Comment