PENIEL Mwingilwa maarufu kama Penny, ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni alinaswa katika picha sehemu akiwa na msokoto mkononi mwake ambao haukuweza kufahamika mara moja kama ulikuwa ni sigara au kitu gani.
Kikizungumza na Amani chanzo chetu makini ambacho ni cha kwanza kuiona picha hiyo akiwa na Halima Kimwana iliyopigwa siku za hivi karibuni, baada ya kusambaa kwa maneno kuwa mtangazaji huyo wa kituo cha televisheni cha DTV alikuwa amepata mshtuko na kulazwa hospitali, kilisema kuwa ‘shemeji’ yetu huyo ni bukheri wa afya.
“Watu wabaya sana, walisema Penny amelazwa baada ya kuziona picha za ‘baby’ wake akiwa eneo la faragha na Wema, si kweli kuna picha ilipigwa siku hiyo ambayo picha za Diamond zimevuja akiwa ameshikilia kitu kama ‘msuba’ vile” kilisema chanzo hicho.
Amani lilimvutia waya Penny, baada ya kujitambulisha na kusalimiana, ghafla alibadilika na kukana jina lake wakati alipoelezwa kuhusu tuhuma za kuonwa kwa picha yake akiwa ameshikilia msokoto.
“Mimi siyo Penny, mimi ni Recho, nahisi utakuwa umekosea namba,” alisikika akijitetea. Lakini baada ya kuulizwa kwa nini mara ya kwanza alilikubali jina lake, hakuweza kuongea tena zaidi ya kuiacha simu yake ikiwa hewani hadi ilipokatwa.


Stori: Shakoor Jongo

0 maoni:

Post a Comment

 
Top