MWENYEKITI wa Simba aliyesimamishwa, Aden Rage, ambaye alisimamishwa wadhifa huo akiwa nje ya nchi, amerejea Dar usiku huu na kusema kwamba yeye bado ni Mwenyekiti halali wa Simba na kwamba kama Kamati iliyomvua wadhifa wake imemwaga ugali, basi yeye atamwaga mboga kesho wakati atakapoongea na wanahabari saa saba mchana. Wadau wa soka na hasa mashabiki wa timu hiyo kongwe ya Msimbazi nchini Tanzania, wanasubiri kwa hamu mkutano huo wa kesho na hatma ya kiongozi huyo mwenye maneno ya kejeli na ambaye pia ni Mbunge wa Tabora mjini kwa tiketi ya CCM.


 
Top