Hatimaye mkutano wa Mwenyekiti aliyesimamishwa Simba, Ismail Aden Rage na waandishi wa habari umefanyika leo mchana kama alivyohaidi jana.

Katika mkutano huo Rage amegoma kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama kama alivyoagizwa na Raisi wa shirikisho la soka nchini Bwana Jamal Malinzi mapema jana.

Akizungumza na waandishi wa habari Rage amesema kwamba haoni sababu za kuitisha mkutano mkuu na endapo TFF na Malinzi wataendelea kumshinikiza kufanya hivyo basi atajiuzulu.


Katika hatua nyingine Rage amemteua mwanachama wa klabu hiyo Michael Wambura kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba.

Pia, amemteua Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini.
 
Top