BONANZA kubwa la NANI MTANI JEMBE ambalo huenda jamii ya Mkoani Ruvuma inaweza kuliita la kihistoria, limefanyika katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea limefanyika jana, ambapo mamia ya wananchi walifurika kwa wingi uwanjani hapo huku mashabiki wa Yanga wakishinda pambano la soka kwa mabao mawili na shindano la kumsaka na kumkimbiza kuku wa kienyeji huku Simba wakiibuka kidedea kwenye mchezo wa kuvuta kamba.
Hali katika uwanja wa Majimaji, maarufu kama wanalizombe ulianza kufurika majira ya saa nne asubuhi, baada ya wananchi hao wengi wakiwa vijana kumaliza shughuli za ibada kutoka makanisani.

Mratibu wa tamasha hilo kwa niaba ya Kilimanjaro Premium Lager, Amedeo Thadeo, alisema kwamba wameamua kufanya bonanza hilo katika mji wa Songea baada ya kubaini kuwa mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa yenye mashabiki wengi wa vilabu vya Simba na Yanga.
Hata hivyo, michezo kadhaa iliyoanza kufurahisha wananchi waliofurika katika uwanja huo ulikuwa wa kufukuza kuku tena Jogoo, ambapo washiriki wawili wapenzi wa klabu za Simba na Yanga walishirikishwa baada ya kuvalishwa jezi za vilabu hivyo.

Lakini kwa bahati mbaya, wapenzi wa Simba, walishindwa kuongeza furaha yao katika uwanja huo, baada ya mshiriki wao kushindwa kumaliza mbio hizo kwa mafanikio, huku yule wa Yanga Deogras Mwanji, akiibuka kidedea baada ya kufanikiwa kumkamata jogoo huyo baada ya dakika mbili na sekunde 25.

Hata hivyo, Mwakilishi wa Mauzo TBL mkoani Ruvuma Masoud Mrisho, aliliambia gazeti hili kwamba mwamko ulikuwa mkubwa uwanjani hapo, baada ya vijana walikuja kutoka Dar es Salaam kufanya maonyesho ya promosheni kadhaa kwenye baa kadhaa mjini Songea.

“Walipokuja hapa Songea wasanii waliosimamia bonanza hili walianza na kuendesha promosheni katika baa ya Serengeti, Yapenda Mtini, Delux II, Mamboleo na kumalizia katika baa ya VALONGO VANGU, mjini Songea na kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa jamii,” alisema Masoud.

Masoud alisema wananchi wengi walikuwa na shauku kubwa la bonanza, hivyo kila kona alikopita yeye na wenzake, walitakiwa kuwahakikishia kwamba bonanza hilo litafanyika bila kukosa, huku wanenguaji kutoka Bendi za Akudo Impact Chicharito, na Afande aka Mjeda na Queen Lucy aka Mama Mdogo wakilipamba jukwaa na kuwaburudisha ipasavyo wananchi waliofurika uwanjani hapo.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kwamba shughuliza kijamii katika mji wa songea zilisimama kwa muda kutokana na bonanza hilo, hali ambayo ilionyesha kuwa wananchi wengi walikuwa na shauku kubwa na bonanza hilo, japo kuwa wasanii wenyeji wa mji wa Songea walishindwa kuonyesha umakini wao baada ya kupatiwa nafasi ya kusherehesha jukwaa.

Waliozungumza na gazeti hili waliipongeza Kilimanjaro Premium Lager kwa bonanza hilo na kusema limeamsha hamasa ya kimichezo mkoani humo, ambayo imepotea baada ya timu ya Maji Maji iliyokuwa ikishiriki Ligi Kuu ya Tanzania kwa miaka kadhaa, lakini ikajikuta ikishushwa daraja baada ya kushindwa kufanya vizuri.

Bonanza hilo lililoshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Joseph Mkirikiti, alionyesha dhahiri ni mshabiki wa Yanga, alipoingia uwanjani alikabidhiwa jezi ya klabu ya Yanga, na aliamua kusalimia wananchi wote kwa kluzunguka na kupunga mikono  na kuamua kwenda moja kwa moja kukaa katika jukwaa kuu la uwanja huo, na kuwapongeza wananchi waliojitokeza katika bonanza hilo akisema amefurahishwa na uratibu wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa shughuli hiyo.

Kikosi cha timu ya yanga


 Umati wa watu wakiangalia michezo iliyo kuwa ikiendelea katika uwanja wa majmaji kushuhudia bonanz kupitia kampeni ya nini mtani jembe.
 Mashabiki wa yanga na simba wanawake wakishindana mchezo wa kuvuta kamba katika bonanza la nani Mtani jembe lililo fanyika katika uwanja wa majimaji.
 Mashabiki wa simba wakishangilia baada ya kuwashinda yanga mchezo wa kuvuta kamba kupitia bonanza la nani mtani jembe 

0 maoni:

Post a Comment

 
Top