DKT. SENGONDO MVUNGI AJERUHIWA VIBAYA, ALAZWA MOI
Posted by GLOBAL on November 4, 2013 at 10:00am
2 Comments
0 Lik Dkt.
Sengondo Mvungi, akiwa kwenye gari la kubeba wagonjwa, baada ya
kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akihamishiwa hapo kutoka
Hospitali ya Tumbi, Kibaha Jumapili Novemba 3, 2013.
Dkt.

KAMISHNA
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania (CRC), Dkt. Sengondo Mvungi,
amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani na usoni, baada ya kukatwa
mapanga, nyumbani kwake, Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya jiji, majira ya
saa sita usiku Jumamosi Novemba 2, 2013.
Kwa mujibu wa taarifa za ndugu na Polisi, Dkt. Mvungi ambaye pia ni
Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria, Chuo Kikuu cha Bagamoyo, mkoani Pwani,
alicharangwa mapanga, baada ya kutaka kujua nini kilichokuwa kikiendelea
kufuatia mabishano baina ya mkewe na watu hao ambao walitishia kumuua
endapo asingewapa fedha.
Taarifa zinasema, watu hao sita wengine wakiwa nje ya nyumba kwa
nia ya kujihami endapo wangevamiwa na majirani, walivamia nyumba hiyo
yenye ghorofa moja, na kumkuta mkewe Dkt. Mvungi wakati huo Dkt. Mvungi
akiwa kwenye chumba tofauti katika nyumba hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, wavamizi walipoona mke wa Dkt. Mvungi
anachelewa kutekeleza maagizo yao, walifyatua baruti na hapo Dkt. Mvungi
akajaribu kuelekea kulikotokea mlio huo na ndipo alipokutana na mapanga
ya kichwani na usoni.
Uchunguzi wa awali wa polisi umeonyesha kuwa tukio hilo ni la
kihalifu, kwani watu hao ambao kwa sasa wanatajwa kama majambazi,
waliiba fedha, simu na laptop, hali inayoonyesha wazi kuwa nia yao
ilikuwa ni kutekeleza wizi.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.SOURCE HAPA
0 maoni:
Post a Comment