Usajili wa Juma Kaseja kujiunga na klabu ya Yanga unafuatia mapendekezo ya benchi la ufundi katika ripoti waliyoikabidhi kwa kamati ya mashindano kwa ajili ya kuboresha kikosi kwa ajili mzunguko wa pili na mashindano ya kimataifa.
Benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Ernie Brandts lilihitaji mlinda mlango mwenye uzoefu wa michezo ya kimataifa kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kimataifa na mzunguko wa pili ambao utakua na upinzani kulingana na kila timu kutaka kufanya vizuri.
Timu yetu imekamilika kila idara, kikubwa tunachokifanya ni kuhakikisha tunazidi kukiboresha na kuyafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi ili kuhakikisha Yanga inaendelea kufanya vizuri na kutisha katika Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
"Najua wegine watajiuliza maswali mengi kwa nini Yanga wamemsajili Kaseja, ukweli ni kwamba walinda mlango waliopo ndani ya Tanzania Kaseja bado ana uwezo nkubwa na msaada ambao atautoa katika kukiimarisha kikosi chetu" alisema Bin Kleb
Kaseja hakua na timu yoyote aliyoichezea katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na timu yake ya zamani ya Simba SC hivyo kujiunga na Yanga kama mchezaji huru katika kipindi hichi cha drisha dogo la usajili.
Kutua kwa Kaseja kunaifanya Yanga kuwa na walinda mlango wanne wote wenye uwezo wa hali ya juu na kutokuwa na shaka wakati wowote timu inapokuwa inakabaliana na mashindao yoyote iwe ni ndani ya nchi au ya nje ya nchi (kimataifa).
Kaseja anaungana na walinda mlango wengine Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul ambao wataitumikia klabu ya Yanga kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom januari 2014 na mashindano ya klabu Bingwa Afika 2014.
0 maoni:
Post a Comment