Paul akipanda stejini



Peter akimsikiliza kaka yake Paul

1Dar es Salaam, 24 Nov 2013 . . Siku ya jumamosi mwezi huu pale leaders club ilikuwa Usiku ya kihistoria kwa tasnia ya burudani nchini Tanzania baada ya wasanii mapacha wa kundi la P Square, Peter na Paul Okoye kutoa burudani ya aina yake ambayo haijapata kutokea kwa muda mrefu hapa nchini kwa maelfu ya mashabiki wa burudani waliojitokeza katika viwanja vya leaders club.
2
Wakiwa ni wasanii wanaokonga nyoyo za mashabiki wa muzikini barani Afrika walisindikizwa na wasanii kutoka hapa nchini ambapo jukwaa lilifunguliwa na msanii Ben Pol ambaye alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki kwa kuimba kwa muziki wa bendi uliokuwa ukipigwa live na bendi ya machozi bendi.
Huku hamu ya mashabiki wa burudani ikianza kukolea kazi iliyofanywa vyema na mwanadada Lady Jay dee iliwatoa jasho mashabiki waliofurika katika viwanja hivyo, huku akiimba wimbo wa joto hasira uliopokelewa vyema na mashabiki ulimshuhudia Profesar Jay akipanda jukwaani huku akichana sehemu ya wimbo huo alioshirikishwa na mwanadada Anaconda.
Kazi ya burudani kwa wasanii wa Tanzania ilifungwa vilivyo na msanii Joh Makini au mwamba wa kaskazini alie limudu jukwaa na kuwapagawisha vilivyo mashabiki wa muziki huku akisaidiwa vyema na msanii mwenzake Niki wa Pili ambao kwa wasasa wanatamba na kibao chao cha tatizo ni bei ya mkaa kilicho pokelewa vyema na mashabiki wao.
Ulifika wakati ambao ulitarajiwa na maelfu wa mashabiki waliojitokea katika viwanja vya leaders club ambapo wasanii Peter na paul okoye, walipopanda jukwaani na kuanza kutoa burudani kwa mashabiki. Wasanii hao walianza kwa kuwashukuru mashabiki waliojitokeza na kuishukuru kampuni ya Vodacom kwa kufanisha ujio wao hapa nchi.
P Square walitoa burudani ya kipekee kwa muda wa masaa mawili mfurulizo bila ya kuchoka na kila walipoweka kibao kingine ndipo moto wa mashabiki ulizidi kuwaka na kukidhi vilivyo kiu ya mashabiki wa burudani.
Burudani ya kipekee ilikuwa pale ambapo wasanii hao walianza kuonesha vipaji tofauti walivyonavyo, huku Peter akionesha uwezo wa kupiga gitaa vilivyo alijibiwa na kaka yake Paul akijibu mapigo kwa kupiga vilivyo ngoma huku wakipokea shangwe kutoka kwa mashabiki wao.
Shukurani za kipekee kwa kampuni ya Vodacom Tanzania iliyofanikisha ujio wa wasanii hawa waliotoa burudani ya kipekee kwa Watanzania hakika itakuwa ni historia ya aina yake kwa tasnia ya burudani na fundisho kwa wasanii wa hapa nchini.
3450066007789 1011121314 15 
 
Top