Muingizaji wa filamu nchini,Jacklyn Wolper amesema pamoja na kuwa na mahusiano na wasanii wenzake akiwemo Diamond,Jux. lakini Ally Kiba ndiye msanii pekee aliyemtambulisha kwenye ulimwengue wa mtamu wa mapenzi.

Akiongea na Global Publishers,muingizaji huyo alisema aliachana na Ally Kiba kwasababu ya wanawake wengi walikuwa wakimtamani kimapenzi.

 ' “Ni kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka. Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima, ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi'Alisema Wolper

“Ali akawa staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tunasalimiana freshi kabisa.”alisema Wolper

 Vipi kuhusu Jux?
  “Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye kabla ya Dallas na yule
mwanaume wangu niliyeachana naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini. Kwa sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana na Jux,”alisema.



“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper.

 
Top