Timu ya Taifa, kilimanjaro Stars Leo imecheza mechi yake ya kwanza ya CECAFA Challenge Cup na timu ya Taifa ya Zambia katika mji wa Machakos, ambao uko takriban kilometa 60 kutoka Nairobi. Timu hizo zimefungana 1-1. Kwa ujumla mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua sana, Katika mechi iliyotangulia ambayo iliwakutanisha Burundi NA Somalia, Burundi iliwafunga Somalia goli 2. Yafuatayo ni matukio katika picha
Hapa vijana wetu wakiwa katika Picha ya Pamoja Kabla ya kwanza kwa kipindi cha kwanza
Bwana shiyo Pamoja na Gavana wa Machakos wakiwasalimia wachezaji.
Mtanange ukiendelea uwanja wa Machakos
Kilimanjaro Stars wakipata dua kabla ya mchezo
Kocha wa Zambia akihojiwa na wanahabari
Mashabiki wa Kilimanjaro Stars wakishangilia timu yao
Wachezaji wetu wakitoka nje ya uwanja baada ya mchezo huo
Makocha wa timu zote mbili wakihojiwa baada ya mchezo