Siku moja baada ya kupokea kipigo cha kihistoria cha 5-0 kutoka kwa Liverpool wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, klabu ya Tottenham Hotspur imemtimua kocha mkuu wa timu hiyo Andre Villas Boas.
Tottenham ambao walikuwa ndio timu iliyotumia fedha nyingi kufanya usajili wakati wa dirisha la usajili, wakitumia zaidi ya paundi millioni 100, wameanza vibaya msimu huu na hivyo kufikia maamuzi ya kumtimua AVB ambaye alijiunga na timu hiyo miezi takribani 18 iliyopita.
Majina ya Luis Enrique na Fabio Capello yameanza kutajwa kuja White Hart Lane kuchukua nafasi inayoachwa wazi na kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Porto.