mwenyekiti wa klabu ya Simba Mh Ismail Aden Rage amesema kwamba hali ya amani ikishindana kutuliza ndani ya klabu ya Simba anatarajiwa kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wote haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kupata uongozi mpya ili kuinusuru klabu hiyo.

Rage ameyasema hayo kwenye kipindi cha SPORTS XTRA cha CLOUDS FM wakati akifanya mahojiano na Alex Luambano kuhusiana na maswala mbali mbali yanaihusu klabu iyo likiwemo la ada ya uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi na klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia,Rage amesema klabu ya Simba bado inaidai pesa hizo Etole na leo hii wametuma faranga za Uswiss 5,000 makao makuu ya shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kama ada ya jaji atakayelishughulikia swala la madai yao.
 
Top