Jana usiku kwa mara nyingine kwenye uwanja wa Old Trafford jijini Manchester wenyeji Man Utd walipoteza mchezo wao kwa changamoto ya mikwaju ya penati mbele ya Sunderland kwenye mchezo wa marudioano wa nusu fainali ya kombe la Capital One.
Hadi dakika dakika tisini zinamalizika Man Utd ilipata ushindi wa bao 1-0 ikabidi ziongezwe dakika 30 za nyongeza kwakuwa kwenye sheria ya goli la ugenini haitumiki kwenye mashindano haya.
Kwenye dakika 30 za nyongeza Sunderland walifanikiwa kufunga bao la kusawazisha kupitia kwa beki wa zamani wa Man Utd aliyepiga shuti kali,dakika chache baadae Javier Hernandez aliifungia Man Utd bao la pili na kupelekea mchezo huo kuamliwa kwa mikwaju ya penati.

Hatimae Sunderland wakafanikiwa kukata tiketi ya Wembley kwenda kukutana na Manchester City kwenye mchezo wa fainali.
 
Top