Pamoja na Cristiano Ronaldo kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia lakini raisi wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesisitiza kwamba kamwe hawawezi kumbadilisha winga wao Franck Ribery na kumchukua mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo.

Winga wa Ufaransa Ribery alishika nafasi ya tatu nyuma ya mshambuliaji wa Real Madrid na Lionel Messi katika kura za Ballon d'or.

Rummenigge anasema hajasangazwa kwamba Ronaldo ameshinda tuzo hiyo lakini bado akasisitiza kwamba Ribery ana thamani kubwa kwao kuliko Ronaldo.

"Mara tu ulipoona kikundi cha watu waliomsindikiza Ronaldo kuja kwenye tuzo kutoka Madrid, haukuhitaji kuwa mtume kujua nini kinafuatia," mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani ya Magharibi aliiambia Bild.

"Lakini Bayern Munich hatuwezi kumbadilisha Frank na Ronaldo."

Rummenigge pia akasema kwamba Mabavaria watafanya kila waliwezalo kuhakikisha wanaendelea kuwa na Mario Mandzukic na Arjen Robben. 
 
Top