Mahakama nchini Spain imeishtaki rasmi klabu bingwa ya nchi hiyo FC Barcelona kwa kufanya udanganyifu wa fedha zaidi ya $12.5 million zilizotumika katika uhamisho wa mshambuliaji wa kibrazil aNeymar. 
Judge Pablo Ruz alisema maamuzi yake yamekuja kutokana kuwepo kwa ushahidi wa kutosha juu ya mashtaka hayo yanayohusiana na uhamisho wa Neymar uliogharimu kiasi cha 57 million euro kutoka Santos msimu uliopita.
Ruz pia ametoa amri ya kuchunguzwa kwa Raisi aliyejiuzulu wa klabu ya FC Barcelona Sandro Rosell juu ya uhamisho huo. 
Rosell alijiuzulu haraka baada ya kugundulika kiasi cha 40 million euros ($55 million) za uhamisho zililipwa kwa kampuni ya baba yake Neymar, ambaye ameitwa kuja kutoa ushahidi mahakamani hapo. 
Barcelona imeyakataa mashataka hayo. 
 
Top