Golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer amewaambia FIFA waachane na adhabu ya mara tatu - penati, kadi nyekundu, na kusimamishwa mechi moja kwa mchezaji ambaye atamzuia mwenzie nafasi ya kwenda kufunga kwa kucheza rafu ndani ya penalty box.


Wakati wa mchezo wa raundi ya 16 bora kati ya  Arsenal na Bayern pale Emirates Stadium, Wojciech Szczesny alimchezea rafu Arjen Robben, na akatolewa nje kwa kadi nyekundu. 
Ingawa David Alaba alikosa penati, Bayern walifanikiwa kushinda 2-0 Szczesny sasa ataukosa mchezo ujao pale Allianz Arena utakaochezwa March 11.
Hata hivyo Neuer anaamini kwamba kusababisha penati ni adhabu tosha - kutoa kadi nyekundu zaidi inakuwa ni adhabu kubwa. 
“Inabidi hili suala waliangalie vizuri, timu inakuwa ishapewa penati, kuongezea kadi nyekundu inazidisha makali makubwa kwa adhabu hiyo. FIFA waliangalie tena hili suala." 
 
Top