Kupitia U HEARDS ya Gossip Cop leo hii, kumekuwa na story ya ugomvi mkubwa uliotokea usiku wa kuamkia leo katika studio zilizopo Maeneo ya Leaders, ambapo mastaa wawili ambao wameurudisha uhusiano wao hivi karibuni "Diamond na Wema" wamejikuta katika ugomvi mkubwa baada ya Ommy Dimpoz kupost Video inayowaonyesha Diamond, Ommy Dimpoz na Victoria kimani wakiwa studio,
Ripoti zinadai kuwa Wema alikuja speed katika studio hizo akiongozana na Aunt Ezekiel, na kuanzisha timbwili akidai kuwa Diamond atakuwa na uhusiano na Victoria Kimani.
Shuhuda wa blog hii aliekuwepo katika eneo la tukio amesema kuwa ngumi zilidum kwa takribani masaa mawili huku Producer Tuddy na Ommy Dimpoz wakihangaika kuachanisha ugomvi huo, Ugomvi huo pia umesababisha Diamond kushika simu ya Wema na kupasua chini huku wakitupiana maneno machafu ya wewe umetembea na fula huku mwingine akimwambia na wewe mbona umetembea na flani na flani, kauli iliyoishia Diamond kumwambia Wema kuwa yeye ndio anamuweka mjini kwa sasa
Tetesi za kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi kati ya the sexy Victoria Kimani na Diamond zilianza kuvuma baada ya kuonekana katika pich aya pamoja wakiwa katika moja ya picha za one project Campaign, ambapo wote walikan akuwa na uhusiano wa kimapenzi.