Raisi wa klabu bingwa ya Bayern Munich Uli Hoeness amejiuzulu kwenye nafasi yake ya uraisi wa klabu hiyo na amesema ameamua kutokata rufaa dhidi ya hukumu aliyopewa.
Hoeness, mmoja watu wazito katika soka nchini Ujerumani, alihukumiwa kwenda jela miaka mitatu na nusu baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi .
Hoeness alisema kupitia taarifa fupi iliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu ya Bayern kwamba amefikia maamuzi hayo baada ya kuzungumza na familia yake na akawaelekeza wanasheria wake wasikate rufaa.