KUNA taarifa zimezagaa kuwa kocha wa Manchester United, David Moyes amefukuzwa kazi, japokuwa haijathibitishwa na familia ya Glazer ambao ndio wamiliki wa klabu hiyo.
Inasemekana familia ya Glazer imefikia maamuzi ya kumfukuza kazi bosi huyo wa Man United ikiwa ni miezi 11 tu tangu arithi mikoba ya Sir Alex Ferguson.
Msemaji wa Man United amegoma kueleza kama kweli Moyes amefukuzwa kazi, lakini imefahamika kuwa kocha huyo hatakuwepo katika mchezo ujao dhidi ya Nowrich City kwenye uwanja wa Old Trafford jumamosi .
Kocha mchezaji Ryan Giggs anatarajiwa kuiongoza Man United mpaka mwishoni mwa msimu, na wakati huo huo wasaidizi wa Moyes Steve Round, Phil Neville na Jimmy Lumsden pia wanatarajiwa kuondoka na bosi wao.
Kocha wa kudumu wa Mashetani wekundu anatarajiwa kutangazwa mwishoni mwa msimu huu.
Familia ya Glazer amechukizwa na kipigo cha jana cha mabao 2-0 dhidi ya Everton na kuwa mechi ya 11 kwa Man United kupoteza katika mashindano yote mwaka huu.
Moyes alisaini mkataba wa miaka 6 mwezi mei mwaka jana kurithi mikoba ya Sir Ferguson aliyestaafu, lakini ameshindwa kupata mafaniko.
Baada ya familia Glazer kufahamu kuwa Man United haitamaliza ligi katika nafasi nne za juu, wameamua kuotesha nyasi kibarua cha Moyes.
Man United wanaelekea kuwa mabingwa watetezi waliofanya vibaya zaidi katika historia ya ligi kuu England kwa kuwa nafasi ya 7 na kwa mara mwisho Ray Harford alifanya hivyo na Blackburn Rovers mwaka 1996. Pia wanatarajia kukosa hata ligi ya Europa msimu ujao.
Bodi ya ukurugenzi ya Man United imekuwa ikimvumilia Moyes kwa matokeo mabaya, lakini walikerwa sana hasa walipofungwa nyumbani na wapinzani wao wakubwa Liverpool na Manchester mwezi uliopita.
Imefahimika hata wachezaji muhimu wa Man United wakiwemo , Robin van Persie, Nemanja Vidic, Rio Ferdinand, Danny Welbeck, Javier Hernandez na Giggs, hawana furaha na Moyes.
Mtandao huu unafuatilia `ngado kwa ngado` kujua hatima ya Moyes.