392295_heroa
KOCHA mkuu wa Bayern Munich, Pep Gaurdiola anaamini klabu yake itakabiliana na changamoto ngumu katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza,  ligi ya mabingwa barani Ulaya hapo kesho dhidi ya Real Madrid.
Timu hizo mbili zitaumana uso kwa uso katika fainali ya kwanza kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu na kocha huyo wa zamani wa Barcelona anaamini kuwa hata kama Cristiano Ronaldo atakosekana, bado hakutaathiri ubora wa wenyeji wao.
“Madrid ni timu ya pekee kwa sasa ikiwa na Carlo Ancelotti. Ni klabu ngumu zaidi tunayokutana nayo katika hatua hii”. Guardiola aliwaambia waandishi wa habari.
“Mara zote ninafurahi kucheza nusu fainali ya UEFA, hususani na timu kama Madrid nikiwa na klabu kama Bayern. Tunahitaji kucheza vizuri na kupata matokeo”.
“Tuna matumaini ya kuonesha burudani kwa mashabiki. Watu wataona mambo mazuri na kama Cristiano atacheza basi wategemee burudani zaidi”.
“Hata kama Ronaldo hayuko fiti, kuna wachezaji wengine wakali kama vile Isco. Bado itakuwa shughuli pevu”.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona anashikilia rekodi ya kutofungwa katika uwanja wa Bernabeu, lakini amegoma kutumia historia hiyo kueleka mchezo wa kesho jumatano.
“Takwimu hizo ni za zamani wakati nikiwa na klabu nyingine na sasa nipo na klabu nyingine. Wala hazina uhusiano na mechi ya kesho”.
 
Top