Chelsea interest in Costa is no surprise - Simeone
Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ametoa ishara kwamba Diego Costa tayari ana ofa kutoka 
Chelsea na akasema kwamba hatomfungia milango mchezaji huyo ikiwa ataonyesha nia ya kutaka kuondoka kwenda Chelsea kupata fedha nyingi Stamford Bridge.
El Confidencial hivi karibuni limeripoti kwamba kocha wa Chelsea Jose Mourinho amepitisha ofa ya 60 million euro kwa ajili ya mhispania huyo wakati wa dirisha la usajili lijalo, huku dili la kumsaini Radamel Falcao likipoteza matumaini.
Simeone aliiambia Al Primer Toque kwamba hashangazwi kuona wachezaji wa Atletico wakizivutia timu nyingi hasa zile kubwa na tajiri.
“[Chelsea] wana nguvu sana kiuchumi.” Tayari wana [Samuel] Eto’o, mchezaji mkubwa, lakini bado wanafikiria kuleta mbadala na Costa anaweza kuwafaa. Anajua kwamba upande mmoja anaweza kupata fedha nyingi zaidi, lakini hapa ataweza kushindana zaidi. Ingenishangaza sana kama timu hizi kubwa zisingekuja kumfuata Miranda [Diego] Godin…
“Ikiwa Costa ataamua kuondoka, itakuwa sawa kwangu. Filosofia yetu siku zote imekuwa kutengeneza wachezaji bora – kwetu sisi huo ni msingi. Wakati Falcao alipoondoka kwenda Monaco, usingeweza kumkatalia kuondoka. Alitupa maisha mpya.”
 
Top