Baada ya kushinda kombe la Europa League mara mbili ndani ya miaka mitano, sasa Atletico Madrid wanataka kwenda steps kadhaa mbele wakijaribu kushinda Champions League kwa mara ya kwanza toka club hiyo ilipoanzishwa takribani miaka 111 iliyopita, na kombe la La Liga kwa mara ya kumi, ikiwa ni takribani miaka kumi na nane imepita toka mara ya mwisho kushinda kombe hilo.
Kudhihirisha kuwa wapo serious kikosi hicho cha Diego Simone tayari kimeweka mkono mmoja kwenye kombe la La Liga huku kikiwaacha Barca na Real Madrid wakiwaombea mabaya kwenye mechi zao zijazo kwani hiyo ndio njia pekee inayoweza kuwakosesha ubingwa. Kwa upande wa Champions League, wamefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali na watapambana na Chelsea katika mechi inayotabiriwa kuwa ya kukata na shoka.
Season hii imekuwa ya mafanikio makubwa kwa Atletico na kuigeuza La Liga kutoka kwenye two team La Liga title race into three. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 14 Atletico wameweza kuwafunga Real Madrid katika Madrid derby ambapo Diego Costa aliipatia bao pekee la ushindi. Mara ya mwisho Atletico kushinda Bernabeu ilikuwa mwaka 1999 waliposhinda magoli 3-1 wakiwa na Jimmy Floyd Hasselbank. Pia kwa season nzima hawajafungwa na Barcelona, wametoa draw katika game zote walizokutana na wakiwafunga katika robo fainali ya UEFA Champions League, wanakutana tena katika game ya mwisho ya kumalizia msimu wa La Liga ambapo kama Barca akishinda basi kuna uwezekano akawa amewapalilia njia Real kuchukua ubingwa na endapo akifungwa itakuwa ni fursa ya Atletico kunyanyua ndoo hiyo ya La Liga, ngoja tusubiri tuone.
Kikosi cha Diego Simone kinaundwa na wachezaji mahiri ambao wana kila sababu za kuiwezesha timu yao kuchukua makombe yote mawili; Ukianzia golini ambaye inasadikiwa kuwa ni the best young goalkeeper in the world ambaye anajitayarisha kui face his own team (Chelsea) Thibaut Courtois ambaye yuko on loan ameweka clean sheets 17 (the most in La Liga this season) and is one of the top three keepers in the world, behind Manuel Neuer and Gianluigi Buffon. The centre-back pair of Diego Godin and Miranda wamekuwa na ukuta imara sana season hii kuweza kumlinda golikipa wao. Katikati tunakutana na Arda Turan, Koke and Raul Garcia ambao wamekuwa na impact kubwa on both fronts. Kwenye upande wa ushambuliaji kikosi hiki kinaundwa na world-class striker David Villa na Spain’s most recent international debutant Diego Costa.
Utamu wa football ndio uko hapa sasa, tunachoweza kusema kwa sasa ni kwamba Chelsea inabidi wajipange hasaaa maana hawa jamaa kwa sasa ni shidaaaa!!!