Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ikiwa katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba leo.
Keptain Msaidizi wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) Frank William akipeana mkono na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba leo .
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia wakiwa wameshikilia Kombe la ushindi la Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC)baada ya timu hiyo kutembelea Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo.
Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ambao ni Bingwa wa Dunia kwa mpira wa miguu kwa watoto wa mitaani wakiwasili nyumbani kwa Waziri Mkuu leo mjini Dodoma mara baada kutembelea Bunge Maalum la Katiba .
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa nahodha msadidizi wa timu ya soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, Frank William, kombe la ubingwa wa dunia wa soka la watoto wa Mitaani wakati alipowaandalia chakula cha mchana kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11,2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Wachezaji wa Timu ya Soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, waliotwaa ubingwa wa Dunia wakipata Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa ajili yao kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11, 2014. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, waliotwaa ubingwa wa Dunia katika Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa ajili yao kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11, 2014. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)