Mtu wa malengo! Louis van Gaal akipozi na mashabiki wakati Uholanzi ikienda kuweka kambi nchini Ureno.
KOCHA mpya wa Manchester United, Louis van Gaal amesema atapiga kinywaji pamoja na Sir Alex Ferguson mara atakapowasili Old Trafford kwa lengo la kurejesha makombe klabuni hapo.Kocha huyo wa sasa wa timu ya taifa ya Uholanzi amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Man united baada ya fainali za mwaka huu za kombe la dunia nchini Brazil.
Van Gaal mwenye miaka 62 ana rekodi ya mafanikio ya kutwaa makombe akiwa na Ajax, Barcelona, AZ Alkmaar na Bayern Munich, lakini atakutana na rafiki yake Ferguson ili kupata maarifa ya namna ya kupata mafanikio katika klabu ya United.
Van Gaal mwenye miaka 62 ana rekodi ya mafanikio ya kutwaa makombe akiwa na Ajax, Barcelona, AZ Alkmaar na Bayern Munich, lakini atakutana na rafiki yake Ferguson ili kupata maarifa ya namna ya kupata mafanikio katika klabu ya United.
Muda wa Maswali: Van Gaal akiongea na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Schipol
Safari imeanza: Van Gaal ataanza kazi Manchester United baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia
Van Gaal amesema atatoka pamoja na Sir Alex Ferguson kwenda kupiga kinywaji baada ya kuwasili Old Trafford.
“Nitatoka naye kupiga kinywaji,” Van Gaal amewaambia Dutch TV.
“Mara nyingi nimefanya hivyo kabla. Sisi ni kama ndugu, na siku zote najipa presha zaidi mwenyewe kabla ya watu kunipa presha”.
Kazi ya kwanza ya Van Gaal ni kurudisha kujiamini kwa United baada ya msimu mbovu waliomaliza katika nafasi ya 7.
Alipoulizwa malengo yake, Van Gaal alisema: ” Man United wanarudi siku si nyingi kama klabu namba moja, mashabiki waanze kuwaza kuwa wao ni mabingwa tena wa England ndani ya mwaka mmoja”.
“Nilifanya hivyo Hispania na Ujerumani. Hata England itawezekana. Nitafurajika sana ikitokea hivyo”. Alisema Van Gaal.