I admire Guardiola, says Luis Enrique
Baada ya kumaliza msimu pasipo kutwaa ubingwa wowote, kocha, Martino aliamua kuachia kazi yake mara baada ya kikosi chake kulazimishwa sare na Atletico Madrid, siku ya jumamosi iliyopita. Baada ya kuisaidia, Barcelona kutwaa taji la Super Coppa kwa sheria ya goli la ugenini dhidi ya Atletico, kocha huyo raia wa Argentina aliifikisha, Blaugrana hatua ya fainali ya kombe la Mfalme, ambayo walipoteza mbele ya mahasimu wao Real Madrid, pia aliisaidia kufika nusu fainali ya michuano ya mabingwa Ulaya, wakitolewa na Atletico, na kumaliza nafasi ya pili katika ligi kuu, La Liga. Martino ameondoka huku timu hiyo ikiwa imepoteza makali yake ya kawaida ndani ya uwanja.
Aliyekuwa kocha wa timu ya Celta Vigo, Luis Enrique Martinez Garcia amepewa kazi hiyo ya kuisuka upya Barcelona ambayo imeshindwa kutwaa taji lolote msimu huu baada ya misimu mitano ya mataji mfululizo. Enlique, mchezaji wa zamani wa timu za Real Madrid na Barca, alianza kazi ya ukocha mwaka 2008, katika timu ya Barcelona B ( timu ya pili ya FC Barcelona), akichukua nafasi ya Pep Guardiola ambaye alikuwa amepandishwa katika kikosi cha kwanza kuchukua nafasi ya Frank Rijkaard, katikati ya mwaka huo. 
Pep, alifanikiwa kwa kiwango kikubwa katika timu hiyo, akishinda mataji 16 katika misimu minne klabuni, Camp Nou. Enlique aliisaidia, Barcelona B kupanda katika ligi daraja la pili baada ya miaka 11. Aliifundisha timu hiyo hadi 2011, na ilipofika, juni 8, akasaini mkataba wa miaka miwili wa kuifunza timu ya AS Roma ya Italia. Kipenzi huyo wa mashabiki wa Barca, Enlique aliondoka Italia mwaka mmoja baada ya kushindwa kuisaidia, Roma kupata nafasi ya kucheza michuano yoyote ya Ulaya. 
Aliamua kurudi, Hispania, na juni 8, 2013 alisaini kujiunga na Celta Vigo ambayo ameisaidia kumaliza katika nafasi ya tisa katika msimu uliomalizika kwa Atletico Madrid kutwaa taji hilo la La Liga…. Wakati wa uchezaji wake, Enlique alishinda taji moja la La Liga katika misimu yake mitano, Real Madrid na alishinda mataji mengine mawili katika klabu ya Barcelona ambayo aliichezea kwa miaka nane, 1996-2004 alipostaafu soka la ushindani akiwa na miaka 34. 
Alicheza michezo 400 na kufunga magoli 104 akiwa na klabu hizo kubwa za Hispania, kiungo huyo wa mashambulizi wa zamani aliiwakilisha timu ya Taifa ya Hispania katika fainali tatu tofauti za kombe la dunia, 1994, 1998, na 2002, alifunga magoli 12 katika michezo 62 ya La Roja
 
Top